Luke 10:25-28

Mfano Wa Msamaria Mwema

25 aWakati huo mtaalamu mmoja wa sheria alisimama ili kumjaribu Yesu, akamuuliza, “Mwalimu, nifanye nini ili niurithi uzima wa milele?”

26Yesu akamjibu, “Imeandikwaje katika Sheria? Kwani unasoma nini humo?”

27 bAkajibu, “ ‘Mpende Bwana Mungu wako kwa moyo wako wote, kwa roho yako yote, kwa nguvu zako zote, na kwa akili zako zote’; tena, ‘Mpende jirani yako kama unavyojipenda mwenyewe.’ ”

28 cYesu akamwambia, “Umejibu vyema. Fanya hivyo nawe utaishi.”

Copyright information for SwhNEN